Thursday, July 31, 2014

Kupata Usajili Rasmi wa Islamic SACCOS of Al-hilaal

Assalaam Alaykum
Habari njema kwa waislam wote na wapenzi wa maendeleo ya waislam kwa Zanzibar na Duniani kote.

iSA inafuraha kukujuilisha kwamba harakati za kutafuta usajili wa iSA zimefanikiwa na kuanzia tarehe 23/07/2014 tumesajiliwa rasmi chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika na kupata nambari ya usajili 5200/2014.

Aidha iSA inawataka wanachama wote wakamilishe taratibu zote za usajili wa uanachama pamoja na kufanya malipo yote yanayolazimu yakiwemo:-
  • Uchukuaji/Urejeshaji wa Application Form
  • Kulipia gharama za kiingilio, TZS 10,000
  • Kuanza kufanya malipo ya HISA, AKIBA na ADA ya kila mwezi
Ni matumaini yetu kufanya Mkutano  Mkuu tarehe 30/08/2014

No comments:

Post a Comment