Sunday, August 31, 2014

Uzinduzi Rasmi wa Ushirika wa Kuweka na Kukopa wa Al-hilaal

Chama cha Ushirika wa Kuweka na Kukopa, kimezinduliwa rasmi tarehe 30/08/2014 katika ukumbi wa Ecrotanal mkabala na Afisi za Huduma za Maktaba, Maisara Mjini Zanzibar.
Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Wajumbe waliosajiliwa rasmi na Asasi wasiopungua 45 na wale ambao hawajakamilisha taratibu za usajili pamoja na wageni kadhaa waalikwa wakiwemo Walimu wa Skuli tofaiti hapa Zanzibar, Wawakilishi wa Asasi nyengine zisizo za Kiserikali pamoja na Asasi za Dini ya Kiislam. Sheha na Ujumbe wake na Wawakilishi kutoka Idara ya Vyama vya Ushirika ambapo kwa pamoja inajumuisha watu wasiopungua 110.
Uzinduzi huo umefanyika chini ya Mgeni Rasmi Mr. Ayman Khalil ambae ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Africa Muslims Agency.
Mgeni Rasmi alikaribishwa na Mlezi wa Asasi ambae ni Dkt. Mohammed Hafidh Khalfan (katika fani ya Uchumi).
Mkutano ulifuatiwa na Ripoti mbali mbali za utekelezaji pamoja na matumizi ya fedha katika kipindi chote cha kuhangaikia Usajili wa Ushirika huo. Pia uliwasilishwa Mpango Mkakati wa muda mfupi (miezi mitatu ijayo) na wa muda mrefu (miaka mitatu ijayo) pamoja na Taratibu/Kanuni za Mikopo kwa Wanachama.

Katika Mkutano huo, Uongozi wa muda ulifanikisha jukumu lake la kufanya Usajili wa Chama pamoja na kuweka mazingira mazuri afadhali ya afisi na taratibu za mtiririko wa matumizi ya fedha na uwekaji wa kumbukumbu za afisi na KUJIUZULU ili kuweka fursa ya kupatikana nguvu kazi mpya katika kusimamia shughuli za kiofisi.
Uongozi wa Zamani (Kamati ya Utendaji) ni kama ifuatavyo:


S/No
Jina
Cheo
1
Mohammed H. Ali
Mwenyekiti
2
Khamis M. Pembe
Katibu
3
Sharif M. Haji
Mjumbe
4
Mohammad M. Abass
Mjumbe
5
Salim A. Salim
Mjumbe
6
Masoud N. Mohammed
Mjumbe
7
Ali R. Ali
Mjumbe















Uongozi wa Sasa ambao utakuwa Umegawanyika sehemu kuu mbili nazo ni:
Bodi ya Islamic SACCOS of Al-hilaal


S/No
Jina
Cheo
1
Khamis Ali Omar
Mwenyekiti
2
Salim Abdullah Salim
M/Mwenyeki
3
Khamis M. Pembe
Mjumbe
4
Mohammad M. Abass
Mjumbe
5
Mohammed Haji Ali
Mjumbe
6
Khamis Othman
Mjumbe
 












Kamati ya Uangalizi wa Shughuli za Asasi


S/No
Jina
Cheo
1
Mohammed Abeid Mbarouk
Mjumbe
2
Amour Omar Mbwana
Mjumbe
3
Nassor Abdallah Rashid
Mjumbe